Ni wakati wa Kabwili kuaminiwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jun 2021
Ni wakati wa Kabwili kuaminiwa

Mwaka juzi wakati Yanga ikinolewa Mwinyi Zahera iliwahi kukumbana na changamoto ya langoni baada ya Beno Kakolanya kugoma

Wakati huo Yanga ilikuwa na walinda lango watatu, Beno, Ramadhani Kabwili na Klaus Kindoki

Kindoki hakuwa akiaminiwa kabisa kwani hakuwa akitabirika langoni

Ndio wakati ambao Ramadhani Kabwili aliaminiwa na kuivusha salama Yanga na kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili msimu wa 2018/19

Msimu huu Kabwili hajapata nafasi ya kucheza mchezo wowote kwenye ligi

Metacha Mnata na Farouk Shikhalo wametumika katika michezo 30, Metacha akicheza mechi nyingi zaidi

Jana Metacha alifanya makosa ambayo yaliwakera mashabiki na baadae akaenda mbali zaidi kwa kuwatusi walipokuwa wakimlaumu kwa kuruhusu mabao mepesi hasa bao la pili kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting

Tayari uongozi wa Yanga umetangaza kumsimamisha Metacha na pengine anaweza asionekane tena akiitumikia Yanga

Shikhalo na Kabwili wanatarajia kumalizia mechi zilizosalia kukamilisha msimu huu

Pengine ni wakati kwa benchi la ufundi kumuamini Kabwili, kwani Wananchi wanaamini anao uwezo wa kuliweka salama lango la Yanga

Alifanya hivyo tangu alipokuwa na umri wa miaka 17, akiweka rekodi ya kucheza mechi ya ligi ya mabingwa katika umri mdogo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’