Mlinda lango Metacha Mnata leo alijikuta katika wakati mgumu mbele ya mashabiki baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2
Ni baada ya kuruhusu bao la pili lililofungwa na David Richard Ollomi kwa shuti la chini chini kwenye dakika ya 82
Mashabiki walishindwa kujizuia kumtupia lawama Metacha ambaye amepoteza imani ya mashabiki kutokana na kauli alizowahi kutoa
Ollomi ni kama alimchungulia eneo alipokuwa hivyo ikawa rahisi kwake kufunga
ADVERTISE HERE