Yanga imefanikiwa kuondoka na alama zote tatu uwanja wa Benjamin Mkapa wakiwachapa maafande wa Ruvu Shooting mabao 3-2
Mabao mawili yaliyofungwa na Fei Toto kwenye kipindi cha kwanza yaliipeleka Yanga mapumziko ikiwa mbele kwa idadi hiyo ya mabao
Hata hivyo kipindi cha pili Ruvu Shooting walikuja juu wakifanikiwa kurejea mchezoni kwa bao la Emmanuel Martin kwenye dakika ya 70
Kuumia kwa kiungo Mukoko Tonombe ni kama kuliathiri safu ya kiungo Ruvu Shooting wakionekana kutawala dakika 20 za mwisho
Saido Ntibazonkiza aliifungia Yanga bao la tatu kwa mpira wa adhabu kwenye dakika ya 80 kabla ya David Richard hajafunga bao la pili kwa upande wa Ruvu Shooting

Presha ilikuwa kubwa wakati mchezo huo ukielekea ukingoni, lakini Wananchi walifanikiwa kuondoka na alama zote tatu
Kulikuwa na tafrani baada ya mchezo kumalizika wachezaji wakitupiana lawama za hapa na pale lakini muhimu wamefanikiwa kuondoka na alama zote tatu
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Mwadui Fc ukitarajiwa kupigwa Jumapili, Juni 20 uwanja wa Benjamin Mkapa