Vijana wa Yanga wametinga fainali ya ligi kuu ya vijana baada ya kuichapa Azam Fc kwa mikwaju ya penati 6-5
Ni baada ya mchezo kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 dakika 120 zikichezwa
Abdulkarim Yunus aliitanguliza Yanga kwa bao safi kabla ya Azam Fc kusawazisha kupitia kwa Ibrahim Issa dakika ya 87
Mchezo haukuwa mwepesi lakini vijana wa Yanga wanastahili ushindi huo kwani walipambana kwa dakika zote 120
Sasa wanamsubiri mshindi wa mchezo kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Simba
Mchezo wa fainali utapigwa Jumamosi, Juni 19
ADVERTISE HERE