Michezo ya nusu fainali ya ligi kuu ya Vijana U20 inapigwa leo ambapo vijana wa Yanga watakuwa dimbani mapema saa nane kuikabili Azam Fc
Yanga ilitinga nusu fainali kibabe kwa kumaliza kinara wa kundi A katika hatua ya nane bora
Suluhu ya bila kufungana dhidi ya Simba, ushindi wa 2-0 dhidi ya JKT Tanzania na ushindi wa 3-0 dhidi ya Mwadui Fc uliwahakikishia Wananchi nafasi kwenye nusu fainali
Yanga wamejipambanua kwa kuwa na kikosi imara kwenye ligi ya vijana
Wana dakika 90 za kusaka nafasi ya kwenda fainali na dakika nyingine 90 za kusaka ubingwa
ADVERTISE HERE