Mambo muhimu mchakato wa Mabadiliko Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
16 Jun 2021
Mambo muhimu mchakato wa Mabadiliko Yanga

Mkurugenzi wa Sheria  klabu ya Yanga Simon Patrick ameainisha mambo matano muhimu ambayo Wanachama na Mashabikim wanapaswa kuyafahamu kuelekea mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Simon ameanisha mambo haya;

1. Yanga kama taasisi iliyoanzishwa mwaka 1935 itaendelea kubaki chini ya Mkutano Mkuu, Baraza la wadhamini, Wajumbe wa kamati ya utendaji, Katibu Mkuu, na Wanachama.

2. Yanga itafungua kampuni ambayo yenyewe itamiliki 51% za hisa zote na kuwaachia wawekezaji 49% za hisa zilizobaki.

3. Kampuni hii mpya kazi yake itakuwa ni kuendesha shughuli za mpira na biashara za mpira tu kwa niaba ya Yanga. Itakuwa na Uongozi wake ambao ni Bodi ya Wakurugenzi, ambao watamuajiri Mtendaji Mkuu, ambaye na yeye ataajiri watendaji wote chini yake kumsaidia kuendesha hii kampuni kama taasisi ya mpira.

4. Kwenye bodi ya Wakurugenzi itakayoanzishwa kusimamia kampuni hiyo kutakuwa na jumla ya wajumbe tisa wa bodi, Yanga itatoa wajumbe watano na wawekezaji kwa ujumla wao watatoa wajumbe wanne

5. Nafasi moja ya ujumbe kwenye bodi itapatikana kwa kununua 12.25 % za hisa, hivyo ili muwekezaji apate nafasi kwenye bodi lazima anunue angalau asimilia hizo za hisa kuingia kwenye bodi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
11h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
16h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
20h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
21h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
21h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
22h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
2d ago
READ MORE →