Takwimu zaibeba Yanga mchezo dhidi ya Ruvu Shooting

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jun 2021
Takwimu zaibeba Yanga mchezo dhidi ya Ruvu Shooting

Msemaji wa Ruvu Shooting Massau Bwire ametamba kuwa timu yake itaondoka na ushindi kesho Alhamisi watakapokutana na Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu

Huo utakuwa mchezo wa pili baina ya timu hizo msimu huu Yanga ikiondoka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza

"Mimi naomba niwaambie Yanga waje na tahadhari hasa mashabiki wale wanaokuja na matokeo yao kuwa iwe isiwe lazima wachukue pointi tatu kwa Ruvu Shooting, mimi niwaambie ni Jambo ambalo halitawezekana na wasije wakaisumbua red cross mara mtu amepeleka macho juu, mara mtu ameanguka na kupoteza fahamu sababu tu ya kile walichokitarajia hakikuwa ivo," alitamba Bwire

Hata hivyo Yanga imepata wastani wa matokeo mazuri kila ilipokutana na Ruvu Shooting katika michezo iliyopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Tangu mwaka 2016 Yanga imekutana na Ruvu Shooting mara tisa kwenye ligi, Wananchi wameshinda mechi saba, Ruvu Shooting wakishinda mchezo mmoja huku mchezo mmoja ukimalizika kwa matokeo ya sare

Yanga imepania kushinda mechi zote tano zilizobaki kuhakikisha hawawapi nafasi watani zao Simba kushinda ubingwa mapema

Kocha wa makipa Yanga Razak Siwa amesema lengo ni kushinda mechi zote zilizobaki na kuwa hatma ya ubingwa itaamuliwa na vile msimu utakavyomalizika

Mchezo utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa muda ukiwa saa moja usiku

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’