Wanachama wa Yanga wametakiwa kuendelea kulipia kadi zao za uanachama ili kuwa sehemu ya historia inayokwenda kuandikwa Juni 27
Siku 11 zimesalia kuelekea Mkutano Mkuu wa Wanachama ambao utabeba ajenda kubwa zenye mustakabali wa klabu ya Yanga
Yanga imedhamiria kufanya Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ambayo yanakwenda sambamba na marekebisho ya Katiba
Wakati huu Wanachama wanaendelea kutoa maoni na mapendekezo yao kabla ya kuelekea katika siku hiyo muhimu
Viongozi wa Matawi nchi nzima walipewa Elimu ya Mchakato huo na wao wanapaswa kuwaelimisha Wanachama katika Matawi yao
Yanga imedhamiria kufanya Mabadiliko yenye tija, Mchakato ni Shirikishi na unafanyika kwa uwazi
ADVERTISE HERE