Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan amekiagiza Chama cha Mapinduzi (CCM) kufanya ukarabati wa viwanja vyote wanavyomiliki kwa kuweka nyasi bandia
Akihutubia vijana katika ziara mkoani Mwanza, Rais Samia amesema sasa michezo ni ajira kwa vijana
Amesema kama CCM hakiwezi kukarabati viwanja hivyo, basi ni vyema wakatafuta wawekezaji wa kufanya kazi hiyo
"Viwanja vingi vya Michezo vinamilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM). Nakiomba chama kikarabati viwanja hivyo na Kama wanashindwa basi watafute wawekezaji ili viwanja viwekwe nyasi za bandia kwani michezo ni ajira," alisema Rais Samia
Hii ni habari njema kwa wadau wa soka nchini kwani kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu juu ya ubora wa viwanja hasa vya mikoani vinavyotumika kwenye ligi za soka nchini