Pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao jana alitoa tahadhari kwa Serikali kutoingilia uchaguzi wa Shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika August 07 mkoani Tanga
Ni baada ya baadhi ya wagombea kulalamikia kanuni zinazotumika kuendesha uchaguzi huo wakiitaka Serikali iingilie kati
Kidau alisema Tanzania inaweza kumbana na rungu la Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kama uchaguzi huo utaingiliwa
Kauli hiyo imewaibua baadhi ya wadau wanaoshangazwa kwani ni mwezi uliopita tu, wao (TFF) walibadili muda wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopaswa kupigwa May 08 kwa sababu ya kupokea maagizo kutoka Serikalini
Yaani TFF walikubali kupokea maagizo ya Serikali kubadili muda wa mchezo ambao baadae ukaahirishwa lakini sasa wanatahadharisha kuwa Serikali ikiingilia uchaguzi Tanzania itafungiwa na FIFA...!