Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kusafiri kwenda Mwanza wakati wowote kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 12 dhidi ya Mbao FC.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye dimba la CCM Kirumba, Jumapili Disemba 31.
Yanga inaondoka jijini Dar es salaam bila kinara wake wa upachika mabao Obrey Chirwa ambaye bado yuko kwao nchini Zambia.
Chirwa alipewa ruhusa na uongozi akiwa ameomba kurudi kwao Zambia kushughulikia matatizo ya kifamilia.
Hata hivyo Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa mgumu.
Mbao FC imekuwa na rekodi nzuri inapocheza katika dimba lake la nyumbani.
Ten amesema wanatambua ugumu wa mchezo huo lakini wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu.
Kukosekana kwa Chirwa ni pigo kwa kikosi cha Yanga ambacho pia kitamkosa Ibrahim Ajib anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano. Donald Ngoma bado ni majeruhi pia.

ADVERTISE HERE