Fiston alia kukosa muda Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jun 2021
Fiston alia kukosa muda Yanga

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Abdulrazak amesema kutopata muda wa kutosha ndio sababu iliyomfanya ashindwe kuonyesha makali yake

Fiston alitua Yanga katika usajili wa dirisha dogo kukiwa na matarajio makubwa kwake

Hata hivyo imekuwa ngumu kwake baada ya kushindwa kupenya kwenye kikosi cha kwanza

Fiston amebainisha kuwa ataondoka baada ya mkataba wake kumalizika

"Nimekutana na changamoto kadhaa tangu nilipojiunga na Yanga. Malengo na maamuzi yangu baada ya changamoto hizi najua mwenyewe ila baada ya kufanya maamuzi ndio nitaweka kila kitu wazi. Kabla ya Yanga kuonyesha nia yoyote binafsi nimetangaza nia yangu siwezi kubaki katika timu hii hata kama wakinihitaji vipi kuongeza mkataba mpya," Fiston aliliambia Mwanaspoti

"Kabla ya msimu kumalizika, niliongea na Kaze nikiwa Misri. Alitaka nije kucheza Tanzania lakini nilimwambia bado nafikiria mbele zaidi kwani nguvu zangu bado zinaruhusu."

"Hata hivyo, aliniambia Yanga inahitaji kumaliza msimu ikiwa bingwa na wanahitaji msaada wangu. Nilimheshimu sana hivyo, niliamua tu kufanya maamuzi ya kujiunga nae na aliniunganisha na Hersi Said na nilisaini na klabu hii"

"Timu haikai pamoja muda mrefu. Mkikaa pamoja mnajuana na kufahamiana vizuri. Wenzetu wanaofanya vizuri ni kwa sababu wachezaji wamekaa muda mrefu pamoja. Ni ngumu kutarajia makubwa kutoka kwa mchezaji wa kigeni ndani ya msimu mmoja na anahitaji muda kuzoea mazingira"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’