Tangu msimu uliopita Yanga inakimbiza soko la mauzo ya jezi ukilinganisha na watani zao Simba
Ni kwa sababu GSM wamekuwa makini sana katika ubunifu wa jezi
Juzi Simba wametoa jezi toleo la tano msimu huu, lakini jezi hizo zimekumbana na ukosoaji kutoka kwa wadau wa soka wakiwemo mashabiki wa klabu hiyo
Msimu unaelekea ukingoni, maandalizi kuelekea msimu wa 2021/22 yameanza GSM wakianza na usajili
Wananchi wanasubiri kwa hamu utambulisho wa wachezaji hao ambao utakwenda sambamba na uzinduzi wa jezi kwa ajili ya msimu ujao
Jambo la uhakika ni kuwa 'mzigo' utakaoshushwa na GSM kila mmoja ataufurahia...!
ADVERTISE HERE