Tambwe apigia mahesabu mabao nane ya Okwi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Dec 2017
Tambwe apigia mahesabu mabao nane ya Okwi
Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe amerejea rasmi kikosini baada ya kuwa nje kwa takribani miezi mitano akisumbuliwa na majeraha ya goti.

Tambwe alifunga bao lake la kwanza msimu huu kwenye michuano ya kombe la FA Jumapili iliyopita wakati Yanga ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Reha FC.

Tambwe amesema ndoto yake ya kutwaa kiatu cha dhahabu msimu huu bado iko palepale na anaamini kama atakuwa fiti katika michezo 18 iliyobaki anaweza kuibuka mfungaji bora.

"Nimerudi vizuri na malengo yangu ni kuisaidia timu yangu kwa kufunga mabao mengi katika ligi kama kawaida yangu ili kuisaidia timu yangu na pia kurejesha Kiatu cha Dhahabu," amefunguka Tambwe.

"Nimekosa mechi nyingi, lakini ligi bado ndio kwanza ipo katikati ya msimu mabao ambayo amefunga anayeongoza naweza na mimi kufunga katika mechi ambazo zimebaki"

Mshambuliaji wa Simba, Emanuel Owki ndiye anayeongoza orodha ya wapachika mabao vinara akiwa na mabao nane.

Anafuatiwa na Obrey Chirwa wa Yanga, Mohammed Rashidi wa Prisons ambao wana mabao sita kila mmoja.

Shiza Kichuya wa Simba, Asante Kwasi wa Lipuli/Simba na Ibrahim Ajib wa Yanga hawa wana mabao matano kila mmoja.

Tambwe anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya kikosi cha Yanga kitakapoivaa Mbao FC jijini Mwanza siku ya Jumapili, Disemba 31.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’