Mwaka 2019 Emmanuel Amunike aliyewahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', alisema kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' ni mchezaji anayeweza kucheza Fc Barcelona klabu ambayo yeye (Amunike) aliwahi kuitumikia
Kauli ile ilibezwa na wengi, lakini kwa hakika ukimfuatilia Fei Toto utabaini ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee
Sasa amekomaa, Tanzania imeanza kunufaika na uwepo wake katika timu ya Taifa
Katika mchezo dhidi ya Malawi leo, Fei Toto alikuwa mhimili kwenye eneo la kiungo, Mwalimu Kim Poulsen akimtumia kwa dakika zote 90
Kama ataendelea kuwa katika ubora na kuongeza juhudi zaidi, sio muda mrefu mwamba huyu ataondoka hapa Tanzania
ADVERTISE HERE