Jana Wazee wa klabu ya Yanga walizungumza na Wanahabari ambapo pamoja na mambo mengine, walilitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kufuata kanuni katika usimamizi wa soka nchini
Mwakilishi wa Wazee alisema baada ya mchezo dhidi ya Simba uliopaswa kupigwa Mei 08 kubadilishwa muda na kupelekea usifanyike, walitarajia TFF wangeeleza sababu ya mchezo huo kubadilishwa muda
Wazee wameeleza kushangazwa na ukimya wa TFF juu ya sababu iliyopelekea muda wa mchezo huo kubadilishwa, badala yake wametangaza tarehe nyingine ya mchezo huo kuchezwa
"Lakini mpaka leo hakuna sababu yoyote iliyotolewa jambo linalotufanya tuone kama tumedharauliwa na kuona wao wanaweza kufanya lolote kwenye mpira wa nchi hii"
"Sasa tunasema hatuwezi kukaa kimya kuona timu yetu haitendewi haki, tunawataka TFF wasimamie kanuni kwa kutupa alama tatu baada ya Simba kutotokea uwanjani Mei 08. Hatuko tayari kucheza Julai 03"
Hivi karibuni Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa alisema kuwa klabu itatoa msimamo wake kuelekea mchezo uliopangwa kupigwa Julai 03 uwanja wa Benjamin Mkapa