Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' jioni ya leo, Jumapili Juni 13, itashuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Malawi ukiwa ni mchezo wa Kimataifa wa kirafiki ambao uko katika kalenda ya FIFA
Kocha Mkuu wa Tanzania Kim Poulsen amesema baada ya kikosi chake kufanya mazoezi ya pamoja kwa siku tisa, wako tayari kuwakabili Malawi
Aidha Poulsen anautumia mchezo huo kama sehemu ya kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu fainali ya kombe la dunia
Mechi hizo ambazo awali zilipaswa kuanza kupigwa mwezi huu, zilisogezwa mbele mwezi Septemba
Mashabiki wa soka nchini wameaswa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuipa sapoti timu yao ya Taifa
Mchezo huo utaanza saa kumi kamili Alasiri

ADVERTISE HERE