Mlinda lango wa Yanga Ramadhani Kabwili amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo baada ya tetesi kuzagaa kuwa ameondoka Yanga
Kumekuwa na taarifa kuwa Kabwili ameshindwa kufikia makubaliano na uongozi wa Yanga kuhusu mkataba mpya na hivyo kuamua kuondoka kambini Kigamboni
Kabwili amesema yeye bado ni mchezaji wa Yanga na hakuna tofauti yoyote iliyojitokeza baina yake na waajiri wake hao
"Habari ya siku hebu niweke wazi maana tangu jana na leo baadhi ya waandishi wa habari na watu tofauti wamekuwa wakinitafuta na kujua kuhusu kuondoka kwangu Yanga na kuhusu mkataba wangu"
"Mimi niwaambie tu mimi bado ni Mwananchi na hakuna tofauti yoyote iliyopo na klabu yangu naishi kwa furaha na Amani kipindi chote kwenye klabu yangu niwaondoe hofu mashabiki wa Yanga," aliandika Kabwili katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii