Kamati maalum iliyoundwa na uongozi wa Klabu ya Yanga kwa ajili ya kusimamia na kuendesha mchakato mzima wa mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu hiyo, imepanga kukutana mwezi ujao kuanza kazi.
Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, chini ya Kaimu Mwenyekiti wake, Clemence Sanga, iliunda kamati hiyo kuratibu mabadiliko hayo ya uendeshwaji wakifuata nyayo za watani zao, Simba.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Alex Mgongolwa, amebainisha kuwa Kamati imepanga kukutana mara baada ya kipindi hiki cha sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
"Tutaanza rasmi kazi baada ya sikukuu ya mwaka mpya, cha kwanza tutakutana kama kamati kupanga nini tutakachoanza nacho kuhakikisha tunafikia malengo yaliyowekwa," alisema Mgongolwa.
Aidha, alisema kuwa kamati yake itahakikisha inatafuta njia ya kuwafikia Wanayanga wote kupata maoni yao juu ya mabadiliko na mfumo sahihi wa kufuatwa ndani ya klabu hiyo.
“Wanachama ndio wenye maamuzi, sisi kama kamati tumepewa tu majukumu yakuhakikisha tunasimamia mabadiliko haya, soka la sasa hivi linaendeshwa kisasa, hivyo ni lazima kuwapo na njia nzuri ya kuiongoza klabu,†aliongezea kusema Mgongolwa.
Alisema wanaamini mchakato huo hautachukua muda mrefu kukamilika.
Simba, ambayo nayo inadhaminiwa na SportPesa, ilipitisha mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu hiyo mwezi uliopita baada ya mchakato wa mabadiliko uliodumu kwa mwaka mmoja ambapo kwa sasa timu hiyo itakuwa ikiendeshwa kwa hisa huku mwanachama Mohamed "Mo" Dewji akinunua hisa asilimia 50 za klabu hiyo.

ADVERTISE HERE