Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera amesema usajili wa mlinzi wa kulia Shabani Djuma aliyetua Yanga kwa dau la zaidi ya Tsh Bilioni moja, umewahamasisha wachezaji wengi wa Kicongo kutamani kuja kucheza soka Tanzania
Zahera ametoa sifa kwa kampuni ya GSM kwa kukamilisha usajili huo ambao inaamika ndio usajili ghali zaidi kuwahi kufanywa na klabu ya Tanzania
Zahera amesema kitendo cha kumsajili Djuma aliyekuwa amewekewa ofa na klabu za Al-Merriekh, Al Ahly na klabu za Afrika kusini, imedhihirisha kuwa GSM hawatanii
"Sasa naona kupitia Yanga na GSM wachezaji wakubwa wa Dr Congo wameanza kutolea macho ligi ya Tanzania ambapo miaka ya nyuma ilikuwa ndoto. Ligi ya Tanzania sasa itakuwa kubwa," Zahera aliiambia EA Redio
Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said bado yuko nje ya nchi akikamilisha usajili wa nyota wa kigeni waliopendekezwa na benchi la ufundi pamoja na Kamati ya ufundi ya Yanga