Fiston 'ajiondoa' kikosini Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jun 2021
Fiston 'ajiondoa' kikosini Yanga

Mshambuliaji Fiston Abdulrazak hataendelea kuitumikia Yanga pale mkataba wake utakapomalizika mwezi ujao

Fiston aliyesajiliwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili, alisaini mkataba wa miezi sita ambao unamalizika msimu utakapofika tamati

Hata hivyo nyota huyo kutoka Rwanda ameshindwa kupenya kwenye kikosi cha kwanza huku kiwango chake kikiwa hakijawashawishi Wananchi

Fiston amesema alikuja nchini kucheza soka lakini baada ya kuona mazingira, hatarajii kuongeza mkataba

"Nilikuja Yanga kucheza soka sio kutembea na mkataba wangu ulikuwa mfupi kwani nilitaka kuyaona mazingira kwanza, lakini kwa muda niliocheza sihitaji tena kuongeza mkataba," alisema Fiston

Fiston ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kutokuwa kwenye mpango wa kocha Nasreddine Nabi kuelekea msimu ujao

Ameifungia Yanga bao moja tu tangu alipotua mwezi Januari mwaka huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’