Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza amerejea kuendelea na majukumu yake baada ya kupona majeraha
Saido alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania na kumfanya akose mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Mwadui Fc
Mchezo ambao Yanga iliweza kupata ushindi na kutinga nusu fainali
Yanga inaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Juni 17 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE