Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya watani zao Simba, vijana wa Yanga watashuka tena uwanjani kesho Jumamosi kuikabili JKT Tanzania
JKT Tanzania walianza vyema nane bora kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui Fc
Wananchi wanahitaji kushinda mchezo huo ili kuwa na nafasi nzuri ya kuweza kuingia nusu fainali
Kocha Mkuu wa vijana wa Yanga Said Maulid 'SMG' amesema vijana wake walicheza vizuri mechi dhidi ya Simba jana lakini walikosa utulivu
"Tumekubali matokeo ya sare lakini tulikuwa na nafasi nzuri ya kushinda. Wachezaji wangu hawakuwa na utulivu walipofika golini. Tutaenda kufanyia kazi changamoto hiyo ili kuhakikisha tunapata ushindi mchezo unaofuata"
ADVERTISE HERE