Zahera afichua Makambo anatamani kurudi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jun 2021
Zahera afichua Makambo anatamani kurudi Yanga

Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera amesema mshambuliaji Heritier Makambo anatamani kurudi Yanga, hata hivyo yeye hahusiki na mpango wa kumrudisha

Gazeti moja la michezo limeripoti kuwa Zahera aliuambia uongozi wa Yanga kuwa anaweza kuwasaidia kumrejesha Makambo kutoka klabu ya Horoya Ac anayoitumikia sasa

Ikumbukwe Zahera ndiye aliyesimamia usajili wa Makambo alipotua Horoya ambako alisaini mkataba wa miaka mitatu, amebaki na mkataba wa mwaka mmoja kunako klabu hiyo

"Taarifa za mimi kutaka kumrudisha Makambo Yanga hazina ukweli wowote kwa sababu mimi sio Wakala wake"

"Lakini nafahamu Makambo anatamani kurudi Yanga, mwenyewe amesema, siku moja atarudi tena Tanzania kuitumikia Yanga," alisema Zahera

Tetesi za Makambo kurudi Yanga zimezidi kushika kasi huku mashabiki wakimtaka Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Injinia Hersi Said kumrejesha mshambuliaji huyo aliyeifunga mabao 21 katika msimu wake mmoja na Yanga

Inaelezwa Horoya Ac wako tayari kumuuza lakini wanataka dau lisilopungua dola 45,000

Yanga ilimuuza Makambo kwenda Horoya kwa dau la dola 80,000 akisaini mkataba wa miaka mitatu na mabingwa hao wa Guinea

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
28m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’