Mabao nane, pasi nne za mabao zinamfanya kiungo mshambuliaji Deus Kaseke kuwa mchezaji aliyetoa mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga msimu huu
Kaseke amechangia mabao 12, akifunga mabao sita na kutoa pasi nne za mabao kwenye ligi, wakati katika michuano ya kombe la FA ameweka kambani mabao mawili
Anashabihiana takwimu na mshambuliaji Yacouba Songne aliyefunga mabao nane na kutoa pasi tano za mabao
Kaseke anastahili kuwa mmoja wa wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Yanga msimu huu
ADVERTISE HERE