Kesho timu ya vijana ya Yanga U20 itashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuwakabili watani zao Simba katika mchezo nane bora ligi kuu ya Vijana
Ni mchezo utakaopigwa kuanzia saa tatu usiku
Baada ya kufanya vizuri kwenye hatua ya makundi, Yanga U20 watakuwa na nafasi nyingine ya kujiweka sawa katika kampeni ya kuwania ubingwa wa ligi ya vijana msimu huu
Kocha wa timu hiyo Said Maulid 'SMG' amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo, wakijipanga kuondoka na alama zote tatu
SMG amesema wamepania kumaliza ubabe wa Mtibwa Sugar kwenye ligi ya vijana
Hii hapa Ratiba ya mechi za U20 ligi ya vijana

ADVERTISE HERE