Fomu za kuwania Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na nafasi tano za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, zinaanza kutolewa leo Makao Mkuu ya TFF pamoja na tovuti ya Shirikisho hilo
Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litafanyika kwa siku tano tu ambapo tarehe ya mwisho ni Juni 12, saa kumi jioni
Mbunge wa Kinondoni na mdau wa soka kwa muda mrefu, Abbas Tarimba huenda akajitosa kwenye kinyan'ganyiro hicho
Tarimba amesema wadau wengi wa soka wamempigia simu huku wengine wakimfuata kumuomba ajitose katika kinyan'ganyiro hicho cha uchaguzi ambao utafanyika August 07 mkoani Tanga
"Kwa sasa bado sijafanya maamuzi, lakini siku tano ni nyingi. Nimepokea maombi kutoka kwa watu wengi wakinitaka niingie kwenye uchaguzi, bado nafanya tathmini kabla ya kufanya maamuzi," alisema Tarimba
Rais wa sasa Wallace Karia anatarajiwa kutetea kiti chake, wapinzani wake watafahamika kuanzia siku ya leo mpaka Juni 12