Kamati ya mchakato wa mabadiliko ya klabu ya Yanga imejipanga kutembea nchi nzima kukusanya maoni ya wanachama wa klabu hiyo
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alex Mgongolwa amesema wamejipanga kuhakikisha mchakato huo unatoa nafasi kwa Wanayanga wengi na Tanzania nzima kutoa maoni yao.
"Lengo ni kufanya mchakato ulio sahihi kitaalamu lakini kuwapa nafasi Wanayanga Tanzania kote kutoa maoni yao.
"Klabu ya Yanga ni ya wanananchi, tunajitahidi kufanya linalowezekana kufanikisha hilo," alisema.
Wiki iliyopita Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga alitangaza Kamati hiyo itakayokusanya maoni kisha kuwasilisha mapendekezo yake juu ya muundo mpya wa uendeshaji wa klabu ya Yanga.
Baadae uongozi wa Yanga utaitisha Mkutano Mkuu wa klabu kupitisha mapendekezo hayo.

ADVERTISE HERE