Morrison aingia 'ubaridi' kesi ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jun 2021
Morrison aingia 'ubaridi' kesi ya Yanga

Mchezaji Bernard Morrison raia wa Ghana ambaye usajili wake wa kujiunga na Simba umepingwa na Yanga, amedai kuwa jitihada zinazofanywa na uongozi wa Yanga ni  kumuondoa asiendee kucheza soka hapa Tanzania

Kesi ya Yanga na Morrison iliyofunguliwa Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa wa Michezo (CAS), inatarajiwa kuanza kusikilizwa wakati wowote huko Uswisi baada ya CAS kutupilia mbali pingamizi lililokuwa limewekwa na Wanasheria wa Morrison waliokuwa wakipinga kesi hiyo kuamuliwa na CAS wakidai kuwa Yanga haikufuata taratibu katika kuifungua

Morrison amedai kuwa anaona jitihada hizo hazilengi kumrejesha Yanga bali ni kumkwamisha asiendelee kucheza soka nchini

"Nahisi viongozi wa Yanga hawataki niendelee kuwepo Tanzania ,wanapambana sana nisiweze kucheza tena soka hapa nchini ", alisema Morrison

Juni 02 ilikuwa tarehe ya mwisho kwa Yanga na Morrison kuwasilisha nyaraka za ziada (kama zipo) kabla ya kesi hiyo kupangiwa tarehe ya kusikilizwa

Kama Yanga itashinda kesi hiyo madhara yake yatakuwa makubwa kwa klabu ya Simba na Morrison mwenyewe

Morrison amesahau kuwa mkataba wa Yanga alisaini mwenyewe! 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’