Mchezaji Bernard Morrison raia wa Ghana ambaye usajili wake wa kujiunga na Simba umepingwa na Yanga, amedai kuwa jitihada zinazofanywa na uongozi wa Yanga ni kumuondoa asiendee kucheza soka hapa Tanzania
Kesi ya Yanga na Morrison iliyofunguliwa Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa wa Michezo (CAS), inatarajiwa kuanza kusikilizwa wakati wowote huko Uswisi baada ya CAS kutupilia mbali pingamizi lililokuwa limewekwa na Wanasheria wa Morrison waliokuwa wakipinga kesi hiyo kuamuliwa na CAS wakidai kuwa Yanga haikufuata taratibu katika kuifungua
Morrison amedai kuwa anaona jitihada hizo hazilengi kumrejesha Yanga bali ni kumkwamisha asiendelee kucheza soka nchini
"Nahisi viongozi wa Yanga hawataki niendelee kuwepo Tanzania ,wanapambana sana nisiweze kucheza tena soka hapa nchini ", alisema Morrison
Juni 02 ilikuwa tarehe ya mwisho kwa Yanga na Morrison kuwasilisha nyaraka za ziada (kama zipo) kabla ya kesi hiyo kupangiwa tarehe ya kusikilizwa
Kama Yanga itashinda kesi hiyo madhara yake yatakuwa makubwa kwa klabu ya Simba na Morrison mwenyewe
Morrison amesahau kuwa mkataba wa Yanga alisaini mwenyewe!
