Ukiachana na cheo cha Rais wa klabu ambacho kitaanza kutumika baada ya Mabadiliko ya mfumo wa Uendeshaji, kutakuwa na Watendaji Wakuu wawili (CEO)
Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said amedokeza mfumo mpya wa uendeshaji utawajumuisha Watendaji hao wawili ambao mmoja atahusika na maswala ya soka tu huku mwingine akihusika na masuala ya kibishara tu
Rais wa klabu atachaguliwa na Wanachama ambao watakuwa wamiliki wa hisa asilimia 51
Kwa upande wa Wawekezaji kutakuwa na Bodi ya Yanga ambayo itakuwa chini ya Kampuni ya Yanga
Bodi itakuwa na wajumbe 9, wajumbe 5 watatoka upande wa wanachama na wajumbe 4 upande wa wawekezaji
Ili kupata nafasi ya kuwa Mjumbe kwenye bodi kwa upande wa Mwekezaji ni lazima uwe na hisa kuanzia asilimia 12.25% ya hizo 49%