Cannavaro afikiri kustaafu mwishoni mwa msimu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Dec 2017
Cannavaro afikiri kustaafu mwishoni mwa msimu
Nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema anakusudia kustaafu mwishoni mwa msimu pale mkataba wake na Yanga utakapomalizika.

Nadir alijiunga na Yanga mwaka 2006 na ifikapo mwaka 2018 atakuwa ametimiza miaka 12 ndani ya kikosi cha Yanga na kuvunja rekodi ya miaka 11 iliyokuwa inashikiliwa na Fred Mbuna.

Nadir amesema hafikirii kujiunga na timu nyingine baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga na zaidi anakusudia kuanza kuhudhuria mafunzo ya awali ya ukocha yanayotolewa na TFF.

Viongozi waandamizi wa Yanga wamekuwa wakimpigia chapuo beki huyo aliyefanikiwa zaidi katika kikosi cha Yanga abaki katika benchi la ufundi pindi mkataba wake utakapomalizika.

Baada ya Yanga kumsajili beki Fiston Kayembe Kanku, nafasi ya Nadir kwenye kikosi cha kwanza imezidi kuwa finyu.

Hata hivyo amekuwa akifanya vizuri kila anapopewa nafasi.

Juzi alitengeneza bao la pili la Yanga kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Reha FC baada ya mpira wake mrefu kutua kichwani kwa Amissi Tambwe.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’