Yanga ya sasa sio sawa na miaka minne iliyopita - Injinia Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jun 2021
Yanga ya sasa sio sawa na miaka minne iliyopita - Injinia Hersi

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, amesema wanayanga wanalo jambo la kujivunia kutokana na maendeleo ambayo klabu imefanya tangu GSM walipoingiza udhamini wao

Injinia Hersi ametoa mfano Yanga ya sasa hakuna tena malalamiko ya mishahara, jambo hilo halikuwepo miaka minne iliyopita

"Tunajivunia maendeleo ya timu yetu, msimu huu hakuna mchezaji anadai timu tofauti na msimu uliopita kuna baadhi ya wachezaji walivunja mikataba na kuondoka mfano Lamine Moro, Lakini tulipoingia tulifanikiwa kumrudisha bado tunaendelea kujenga timu yetu," Injinia Hersi aliiambia EFM

Hersi pia amezungumzia usajili ambao Yanga imefanya kuwa ni bora zaidi ukilinganisha na miaka minne nyuma

"Hata kwenye usajili tumefanya mambo makubwa. wachezaji tuliowasajili wana ubora wa hali ya juu. Angalia wachezaji kama Mukoko Tonombe ameitwa timu ya Taifa akitokea Yanga. Kuitwa timu ya Taifa ya DR Congo sio jambo dogo"

"Wachezaji kama Yacouba Songne, Yassin Mustafa wameitwa timu ya Taifa kwa mara ya kwanza wakitokea Yanga"

"Timu haijengwi kwa siku moja, tunaendelea kuijenga timu yetu. Tunaleta wachezaji wazuri zaidi msimu ujao, wale ambao wameshindwa kufanya vizuri tutaachana nao," alisema Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’