Juzi Juni 02 ilikuwa tarehe ya mwisho kwa Yanga na Bernard Morrison kuwasilisha vielelezo vya ziada kabla ya kesi yao kuanza kusikilizwa
Awali kulikuwa na pingamizi la Morrison ambaye alitaka kesi hiyo irejeshwe Tanzania kwa hoja kuwa Yanga hawakupaswa kufungua kesi CAS moja kwa moja baada ya hukumu ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji
Walipaswa kuomba mrejeo 'Review' ya kesi hiyo kwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambayo ndio iliyobatilisha Mkataba wa Morrison na Yanga
Pingamizi hilo lilitupiliwa mbali na CAS baada ya Mahakama hiyo ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo kujiridhisha kuwa wanayo Mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo
Hivyo pande zote wakapewa mpaka kufikia juzi wawe wamewasilisha vielelezo zaidi (kama vipo) kabla ya kesi hiyo kupangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa
CAS bado hawajatangaza tarehe ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa. Lakini itakapokuwa tayari itawekwa kwenye mtandao wao HAPA