Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli ametoa ufafanuzi wa kauli aliyoita juzi kuhusu mchezo dhidi ya Simba uliopangwa kupigwa Julai 03 2021
Bumbuli amesema Yanga inautambua mchezo huo, watacheza kama ratiba inavyoonyesha
Bosi huyo wa kitengo cha Habari na Mawasiliano amesema kauli aliyotoa juzi ni sehemu ya utani wa jadi
Amesema, kwa kutambua kuwa mchezo huo ni wa kiporo, maandalizi yake yaliisha Mei 08, kwa sasa wanajiandaa na mechi nyingine nne ambazo sio viporo
"Tunatambua kuwa mechi ipo kama ilivyopangwa kwenye ratiba, mimi nilichokuwa nazungumzia ni kwamba sisi tuna maandalizi ya mechi nne ambazo ni 'fresh match'. Maandalizi ya mechi ya Simba yaliishia tarehe nane, kilichopangwa kwenye ratiba ni kiporo"
"Sasa kiporo maandalizi yake ni kuwa hata ukichemsha unakula. Ndio maana nikasema hii mechi hata tukiamshwa usiku wa manane, tunacheza"