Nyota wa ndani wa kuangaliwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jun 2021
Nyota wa ndani wa kuangaliwa

Tathmini ya wachezaji wazawa ambao wanaweza kuongezwa katika kikosi cha Yanga kuelekea msimu ujao

Yanga imejipanga kuboresha kikosi chake, zoezi ambalo mabosi wa Kamati ya usajili wameshaanza kulifanya kwa umakini mkubwa

Wapo wachezaji wa ndani ambao waliofanya vizuri msimu huu, miongoni mwao hawa wamejipambanua;

Yusufu Mhilu

Mshambuliaji wa Kagera Sugar Yusufu Mhilu kwa sasa ni miongoni mwa washambuliaji wa ndani walio katika kiwango bora sana

Msimu huu kwenye ligi Mhilu amefunga mabao tisa, haishangazi kuona kocha Kim Poulsen amemjumuisha kwenye kikosi chake cha timu ya Taifa kinachotarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe Juni 13

Wakati Yanga ikiwa katika mchakato wa kuimarisha safu yake ya ushambuliaji, kwa wachezaji wa ndani Muhilu anaonekana kuwa chaguo sahihi zaidi

Habari njema ni kuwa huyu ni mchezaji aliyekulia ndani ya Yanga. Aliondoka akiwa chipukizi lakini sana amekomaa

Msimu uliopita alifunga mabao 13 na msimu huu upo uwezekano mkubwa atafunga mabao zaidi ya 10

Rajabu Athumani

Ni kiungo mshambuliaji anayeitumikia klabu ya Gwambina Fc

Pamoja na Gwambina kuwa katika hatihati ya kuteremka daraja, Rajabu ndiye mchezaji bora wa timu hiyo msimu huu

Nyota huyo ana pasi saba za mabao. Ni mchezaji ambaye anaweza kuongeza kitu kwenye kikosi cha Yanga msimu ujao

Abdulmajid Mangalo

Kama Yanga itahitaji kuongeza mlinzi wa kati, basi ni huyu Abdulmajid Mangalo

Kabla ya Dickson Job kusajiliwa dirisha dogo, Mangalo alikuwa akitajwa zaidi

Akiwa nahodha wa Biashara United, Mangalo ni mmoja wa wachezaji walioifanya Biashara United iwe imara sana

Biashara United watacheza na Yanga mchezo wa nusu fainali kombe la FA na pia wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi

Nao wanawania nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao

Bryson David

Yanga inatajwa kuwa na mpango wa kuongeza mlinzi wa pembeni upande wa kushoto

David Bryson wa KMC anaweza kuwa ndio mchezaji aliyefanya vizuri zaidi katika nafasi hiyo msimu huu

Inaelezwa Yanga imemuulizia kwa klabu yake ya KMC.Anaweza kuwa usajili wa faida sana kuelekea msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’