Jana Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli alifichua kuwa Yanga haitambui mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopangwa kupigwa Julai 03 2021
Ni baada ya mchezo uliopaswa kupigwa May 08 kuahirishwa katika mazingira ya kutatanisha
Yanga iliingiza timu uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni muda ambao mchezo huo ulipaswa kupigwa
Bumbuli amesema kwa sasa Yanga inafanya maandalizi kwa ajili ya kukamilisha michezo minne ya ligi pamoja na kombe la FA
"Sisi tuna michezo minne iliyobaki dhidi ya Ruvu Shooting, Mwadui Fc, Ihefu na Dodoma Jiji. Mchezo dhidi ya Simba ulikuwa May 08 sisi tulifika uwanjani lakini wenzetu hawakutokea. Mchezo huo umeshapita," alisema Bumbuli
Yanga imekuwa na mvutano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiwa na malalamiko ya kutotendewa haki katika masuala kadhaa
Zipo hoja, Yanga ndio klabu iliyoadhibiwa zaidi na TFF msimu huu kwa kile kinachoelezwa kuwa viongozi na mashabiki wake wanakiuka kanuni za uendeshaji wa soka nchini
Lakini kwa hili la mchezo dhidi ya Simba wako salama kwani wamefuata kanuni