Dominic Albinus ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga.
Kamati hii inahusika moja kwa moja na michakato ya usajili kwani mchezaji yeyote anayependekezwa kusajiliwa lazima jina lake lipite katika Kamati hii
Albinus amesema kuwa anayo majina kadhaa ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa msimu ujao lakini hakuna jina la kiungo wa Simba Ibrahim Ajibu
Albinus amefunguka kuwa katika usajili wao, yapo mambo kadhaa wanayoyazingatia na kuwa wanamsajili mchezaji kwa kuangalia kile anachofanya wakati huu na sio wakati uliopita
"Hatuwezi kumsajili Ajibu kwa historia yake makosa ya namna hiyo hayawezi kufanyika sasa, hajacheza karibu msimu mzima, mchezaji wa ndani tutakayemsajili kila mtu atakubali takwimu zake kwa kile ambacho amekifanya ndani ya msimu mmoja unaoisha au zaidi"
"Tutasajili wachezaji bora msimu ujao, ni kazi ambayo tulianza muda mrefu, tunafahamu usajili wakati mwingine ni kama kamari lakini safari hii tutakuwa makini zaidi tunajua shida ya kikosi chetu," alisema Albinus
"Tunaheshimu uwezo wa Ajibu lakini ni vigumu kutetea usajili wake kwa mtu ambaye kocha hajamuona akicheza , msimu mzima amekuwa akisotea benchi"