Klabu ya Yanga imemrejesha kazini aliyekuwa Kaimu katibu Mkuu na Mwanasheria wa klabu Simon Patrick baada ya kamati iliyoundwa kuchunguza tuhuma dhidi yake kutomkuta na hatia
Taarifa iliyotolewa na Yanga, imebainisha kuwa ripoti ya kamati iliyoongozwa na Wakili Raymond Wawa haikubaini ukweli wowote wa tuhuma zilizoelekezwa kwa Wakili Simon na hivyo Kamati ya Utendaji imejiridhisha kuwa Simon hakuwa na hatia katika tuhuma zilizopelekea akasimamishwa kazi Novemba 18 2020
Rasmi Yanga imemrejesha Wakili Simon katika nafasi yake ya Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama kuanzia May 30 2021
Wakili Simon alikuwa mmoja wa Wanasheria wa Yanga waliosimamia kesi dhidi ya Bernard Morrison, amerejea kukamilisha kazi
Kesi itaanza kuunguruma Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa Michezo (CAS) baada ya Mahakama hiyo kutupilia mbali ombi la mshitakiwa Bernard Morrison aliyeomba kesi hiyo irejeshwe Tanzania baada ya kudai Yanga wamekiuka taratibu katika kuifungua
Aidha leo ndio siku ya mwisho kwa Yanga na Morrison kuwasilisha nyaraka zaidi (kama zipo) kabla ya hukumu kutolewa na CAS