Hakuna mafanikio bila ya nidhamu - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jun 2021
Hakuna mafanikio bila ya nidhamu - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema jitihada za kutengeneza kikosi imara haziwezi kufanikiwa kama suala la nidhamu halitazingatiwa

Takribani mwezi mmoja tangu alipojiunga na Yanga, Nabi amejipambanua kwa kuwa na msimamo katika kusimamia nidhamu ya wachezaji

Kocha huyo raia wa Tunisia amesisitiza kuwa malengo hayawezi kutimia kama hakutakuwa na nidhamu. Ameeleza kuwa kila mchezaji anapaswa kuzingatia hilo na kwamba nyota waliokutana na adhabu ni mfano kwa wengine ambao wana tabia za kujiona wakubwa kuliko klabu

"Tangu nimekuja hapa nimekuwa nikifuatilia mienendo ya wachezaji wangu, nataka kujenga kikosi imara kitakachoogopeka Afrika, nitafanikiwa katika hilo iwapo suala la nidhamu  litakuwa vizuri," alisema Nabi

"Nami nitasimamia hilo bila kuangalia kiwango cha mtu,  anayeweza kufuata matakwa ya klabu tutaendelea kuwa naye, atakaeshindwa kuendana na kasi yetu milango iko wazi, malengo yetu ni kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa hapo mwakani"

Aidha kuhusu kikosi chake, Nabi amesema anahitaji kufanya marekebisho kadhaa ili kuendana na ukubwa wa timu kwa kufanya usajili wa wachezaji wenye uwezo mkubwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’