Baada ya mapumziko ya mwezi mmoja kupisha michuano ya CECAFA Chalenji na kombe la FA, ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 12 inatarajiwa kuendelea Ijumaa, Disemba 29.
Ijumaa Azam FC itakuwa mwenyeji wa Stand United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1:00 usiku huku Jumamosi, Disemba 30 zikitarajiwa kupigwa mechi tatu.
Lipuli na Tanzania Prisons Uwanja wa Samora, Iringa kuanzia Saa 8:00 mchana, Mtibwa Sugar na Maji Maji Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Ndanda na Simba, zote saa 10:00 jioni.
Jumapili, Disemba 31 mabingwa watetezi, Yanga watakuwa wageni wa Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza saa 10:00 jioni na Njombe Mji FC wataikaribisha Singida United kuanzia saa 8:00 mchana Uwanja wa Saba Saba, Njombe.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa 12 zitachezwa mwaka mpya, Januari 1 Mbeya City wakiikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Mwadui wakiikaribisha Ruvu Shooting zote kuanzia saa 10:00 jioni.
Baada ya mechi hizo, Ligi Kuu itasimama tena kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar na raundi ya tatu ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayochezwa kati ya Januari 5 na 7 mwakani kabla ya kuingia kwenye mzunguko wa 13 wa ligi kuanzia Januari 13 na 17, 2018.

ADVERTISE HERE