Serikali iisafishe TFF - Tarimba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 May 2021
Serikali iisafishe TFF - Tarimba

Mbunge wa Kinondoni (CCM) Abbas Tarimba ameishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulisafisha Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ili kuleta matumaini yaliyotarajiwa na wapenzi wa soka nchini

Tarimba ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 31, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Mchezo kwa mwaka 2021/2021

Tarimba amesema kumekuwa na malalamiko kutoka viongozi wa klabu wanaopewa adhabu zisizo na usawa

"Leo huyu akifanya makosa yale yale anapona mwingine leo akifanya makosa yale yale anaadhibiwa kesho yake na adhabu za kutisha zaidi," alisema

Aidha, Tarimba aliongeza kwa kusema kuwa hata waamuzi wamejiingiza katika mambo hayo hayo kwa kufanya upendeleo uwanjani jambo ambalo linazikosesha klabu nyingine ushindi kwasababu waamuzi wanaogopa watafungiwa

"Malalamiko yanapelekwa TFF leo kesho yapatiwa majibu, mengine yanakaa miezi sita hadi saba, standard (usawa) iko wapi? napata mashaka ndani ya TFF hakuna uadilifu"

Amehoji wanataka kuonyesha nini kwasababu mahusiano mabaya yanafikia hadi kati ya mtu na mtu na kutoa mfano wa kiongozi aliyekataa kupokea mkono hivi karibuni.

Ameitaka Serikali kusafisha mpira wa miguu ili kuleta matumaini yaliyotarajiwa na kwamba mambo hayo yameathiri hata timu za Taifa ambazo hazina matumaini

Tarimba pia aligusia kitendo cha TFF kusogeza muda wa mchezo kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopaswa kupigwa Mei 08 bila ya kujali uwekezaji mkubwa uliokuwa umefanywa na vilabu pamoja na wadau wengine wakiwemo mashabiki waliokuwa wamelipa fedha kwa ajili ya kuushuhudia mchezo huo ambao haukufanyika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
49m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’