Baada ya uongozi wa Yanga kutangaza kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wa kiungo Carlos Carlinhos raia wa Angola, wapo mashabiki wameonyesha wasiwasi isije ikatokea nyota huyo akaibukia upande wa pili
Hata hivyo viongozi wa Yanga wamekuwa makini, wakati huu wakiwa bado wanapambana na kesi ya winga Bernard Morrison, wangefanya makosa makubwa sana kama wangemuacha Carlinhos aondoke hivihivi
Inaelezwa katika makubaliano ya kuvunja mkataba wake, Yanga imeweka kipengele cha fidia ya dola 200,000 (Sh.480 milioni) kama atarejea nchini kujiunga na klabu nyingine ndani ya kipindi cha miaka minne
Hii ina maana kama Carlinhos atarejea Tanzania kujiunga na timu yoyote ndani ya muda huo, Yanga itavuna Tsh Milioni 480
Kama sivyo basi timu yoyote itakayomnuhitaji kujiunga nayo nje ya gharama za Yanga italazimika kusubiri mpaka mwaka 2025