Wakati Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) jana likitoa taarifa ya kuagiza ufanyike ukaguzi wa viwanja vilivyochaguliwa kutumika kwenye michezo ya nusu fainali na fainali ya kombe la Shirikisho (ASFC), Wanachama wa Yanga mkoani Tabora wamejitosa kuboresha uwanja wa Ali Hassan Mwinyi
Uwanja huo ulichaguliwa kutumika kwenye mchezo wa nusu fainali kati ya Yanga dhidi ya Biashara United

Katika taarifa yake jana, TFF ilibainisha kuwa inaweza kubadili viwanja hivyo kama watajiridhisha haviko tayari kutumika
Mchezo mwingine wa nusu fainali kati ya Simba dhidi ya Azam Fc umepangwa kupigwa uwanja wa Majimaji Songea wakati mchezo wa fainali umepangwa kupigwa uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma
ADVERTISE HERE