Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema anahitaji kuona timu yake inashinda michezo yote mitano iliyobaki ili kukusanya alama 15 ambazo zinaweza kuwapa nafasi ya kushinda ubingwa wa ligi kuu msimu huu
Yanga imesalia na michezo mitano kukamilisha msimu dhidi ya Mwadui Fc, Ihefu Fc, Ruvu Shooting, Simba na Dodoma Jiji
Kwa sasa ligi imesimama kupisha mechi za Kimataifa ambazo ziko kwenye kalenda ya FIFA
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Ruvu Shooting ukitarajiwa kupigwa Juni 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
"Ligi bado inaendelea hivyo tunapaswa kuwekeza nguvu kwa kila mashindano tunayoshiriki ili kutwaa mataji kama malengo yetu tuliyojiwekea."
"Nawapongeza wachezaji wangu kwa kile ambacho wamekuwa wakikifanya wamepambana sana, naamini tunaenda kutimiza malengo yetu japokuwa naamini haitakuwa jambo rahisi lakini kama tutatimiza mipango kila kitu kinawezekana," alisema Nabi.
Kocha huyo raia wa Tunisia amesema licha ya kujiunga na Yanga msimu huu ukiwa unaelekea ukingoni, lakini anajua kiu ya mashabiki ni kuona inafanya vizuri na kushinda mataji na wao wataendelea kupambana ili kutimiza malengo yao ya msimu.