Nabi ampa mtihani Lamine

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 May 2021
Nabi ampa mtihani Lamine

Hivi karibuni nahodha wa Yanga Lamine Moro aliingia kwenye mgogoro na benchi la ufundi na kupelekea nyota huyo aondoshwe kambini Mtwara wakati Yanga ikijiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc

Tayari uongozi wa Yanga umepata suluhu ya sintofahamu hiyo kati ya Lamine na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Nasreddine Nabi

Kumekuwa na maswali kama Kocha Nabi ataendelea kumkabidhi Lamine kitambaa cha unahodha au la

Nabi amebainisha kuwa bado ana imani na Lamine kuendelea kuwa nahodha wa timu lakini akimtaka ajitathmini na kuwa mfano kwa wachezaji wengine

"Sioni kama tutafanya uamuzi huo, Lamine alikosea na ana nafasi ya kubadilika, atabaki na nafasi yake. Kitu anachotakiwa ni kuhakikisha anabadilika ili awe mfano bora kwa anaowaongoza"

"Ukiwa kiongozi wapo ambao watakuangalia kwa kile unachofanya na ndio maana amekosea na atapewa adhabu, kuanzia hapo anatakiwa kubadilika na kuwa kiongozi wa mfano mzuri,” alisema Nabi.

Lamine anatarajiwa kurejea kikosini sambamba na Metacha Mnata na Michael Sarpong baada ya mapumziko ambayo wachezaji wamepewa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’