Timu zilizofuzu 32 bora ASFC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Dec 2017
Timu zilizofuzu 32 bora ASFC
Timu 12 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, 11 za Daraja la Kwanza, tatu za Daraja la Pili na nne za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa zimefuzu hatua ya 32 ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inasubiriwa kutoa maamuzi juu ya mechi mbili kati ya Abajalo ya Daraja la Kwanza dhidi ya Tanzania Prisons na Mvuvumwa (Daraja la Kwanza) na JKT Ruvu Ligi Kuu ambazo hazikufanyika katika hatua ya 64 Bora kutokana na baadhi ya wachezaji kukosa leseni.

Na hiyo ilitokana na mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) unaojulikana kama TMS kufeli hali iliyosababisha klabu kushindwa kukamilisha usajili kwa wakati kupitia mfumo huo.

TFF iliagiza klabu ziwasilishe moja kwa moja usajili wake makao makuu ya shirikisho, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ingawa siku moja kabla ya kuanza mechi za hatua ya 64 Bora ASFC mfumo huo ulifunguliwa tena baada ya marekebisho ya hitilafu zilizojitokeza kufuatia shirikisho hilo kuwasiliana na waendeshaji wa mfumo huo walioko Tunis, Tunisia na klabu zikatakiwa kuendelea kusajili hadi Desemba 23 dirisha lilipofungwa tena.

Timu za Ligi ya Mabingwa wa mikoa zilizofuzu ni Buseresere FC ya Geita, Majimaji Rangers ya Nachingwea, Lindi, Kariakoo United ya Lindi Mjini na Shupavu FC ya Morogoro, wakati za Daraja la Pili ni Green Warriors ya Dar es Salaam iliyowatoa mabingwa watetezi, Simba, Ihefu FC ya Mbeya iliyoitoa Mbeya City na Burkina Faso FC ya Morogoro iliyoitoa Lipuli ya Iringa.

Timu za Daraja La Kwanza ni Toto Africans ya Mwanza, KMC, Polisi, Friends Rangers za Dar es Salaam, Polisi Tanzania ya Morogoro, Rhino Rangers ya Tabora, JKT Oljoro ya Arusha, Biashara United ya Mara, Pamba SC ya Mwanza, Kiluvya United ya Pwani na Dodoma FC ya Dodoma.

Timu za Ligi Kuu ni pamoja na makamu bingwa, Mbao FC ya Mwanza, Ndanda FC ya Mtwara, Njombe Mji ya Njombe, Kagera Sugar ya Bukoba, Stand United ya Shinyanga, Singida United ya Singida, Ruvu Shooting ya Pwani, Mwadui FC ya Shinyanga, Maji Maji FC ya Songea, Azam FC, Yanga SC za Dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Droo ya hatua ya 32 Bora inatarajiwa kupangwa wiki ijayo Γ’β‚¬ΛœliveÒ€ℒ katika studio za Azam TV, Tabata mjini Dar es Salaam.

Bin Zubeiry<
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’