Mechi ilipaswa kupigwa May 08, saa 11 jioni. Masaa mawili kabla ya mchezo, inatolewa taarifa na TFF kuwa muda umesogezwa mbele pasipo kutolewa sababu
Wananchi wanapinga mabadiliko hayo ya 'kienyeji' na kuingiza timu uwanjani saa 11 kama ratiba ilivyokuwa ikieleza
Bado kuna watu wanaaminishwa kuwa Yanga iliikimbia Simba May 08 wakati kila mmoja aliwaona Wananchi wakiingia uwanjani katika muda sahihi
Na kama Yanga ilikimbia kwa nini TFF inapanga tena tarehe nyingine ya mechi kuchezwa?
Kanuni na taratibu si zinafahamika kwa timu ambayo haikufika uwanjani?
Hiyo Julai 03 inakujaje tena wakati mnasema Yanga ilikimbia? Si chukueni pointi tatu na muwashushe Yanga madaja mawili?
Halafu baada ya hapo ndio itafahamika kipi kinapaswa kufuatawa kanuni au maagizo!
Busra na heshima kwa Tanzania ndio vinaifanya Yanga kuridhia kucheza mechi ya Julai 03 . Lakini kama wakiamua wasiingize timu, hao wanaopiga makelele ya kukimbiwa watakuwa wa kwanza kulia
Mnataka kuwaaminisha watu sisi tulikimbia, guys acheni hizo, sisi tulifika, wenzetu hawakutokea. Kama tulikimbia #Kanuni ziko wazi zitumike. #Taarabu zenu tukizichoka tutaweka verse yetu ya #HipHop. Tulichagua kukaa kimya kwa maslahi ya ??
— Hassan Bumbuli (@HBumbuli) May 27, 2021