Mlinda lango Farouk Shikhalo jana alikuwa katika kiwango bora sana kwenye mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Mwadui Fc uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-0
Farouk alirejea langoni akipishwa na Metacha Mnata ambaye alikosekana kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu
Katika mchezo huo Shikhalo aliokoa takribani mashambulizi matatu ya hatari ambayo yangeweza kuwapatia Mwadui Fc bao
Shikhalo ni mmoja wa wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu, hajawahi kuingia kwenye mgogoro wowote na Yanga licha ya kupita katika nyakati tofauti tofauti
Ni miongoni mwa wachezajiwa kigeni waliosajiliwa na Mwinyi Zahera misimu miwili nyuma, kikosini akibaki yeye na Lamine Moro
Wakati anatua Yanga Shikhalo alisajiliwa sambamba na akina Juma Balinya, Sadney Urikhob, Mybin Kalengo, Mustafa Selemani, Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, David Molinga na wengine ambao hawapo tena Yanga