Ushindi wa mabao 2-0 ambao Yanga walipata dhidi ya Mwadui Fc jana, umewapeleka Wananchi nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Kituo kinachofuata sasa ni mkoani Tabora uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ambako mchezo wa nusu fainali dhidi ya Biashara United utachezwa
Huu ni msimu wa tatu mfululizo Yanga inatinga nusu fainali. Misimu miwili nyuma wananchi waliishia hatua hiyo lakini msimu huu vijana wa Nasreddine Nabi wanalitaka kombe la FA
Wakivuka nusu fainali, safari ni mkoani Kigoma uwanja wa Lake Tanganyika ndiko mchezo wa fainali utapigwa
Jambo jema zaidi kwa Wananchi ni kuwa timu yao sasa imeanza kuonesha utofauti mkubwa, kandanda safi linapigwa huku nafasi za mabao zikitengenezwa kwa wingi
ADVERTISE HERE